• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani na Russia wajadili masuala ya Ukraine na Syria kwa njia ya simu

    (GMT+08:00) 2017-12-28 09:59:29

    Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema mawaziri wa mambo ya nje wa Marekani na Russia Bw. Rex Tillerson na Bw. Sergei Lavrov wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu kuhusu masuala ya Ukraine, Syria na Peninsula ya Korea.

    Taarifa imesema Bw. Tillerson amefuatilia kupamba moto kwa matukio ya matumizi ya mabavu yaliyotokea mashariki mwa Ukraine, akitumai kuwa Russia itarejea katika kituo cha kusimamia na kuratibu usitishwaji vita na utulivu, ili kupunguza hali ya wasiwasi.

    Pande hizo pia zimesisitiza kuunga mkono mazungumzo ya amani ya Geneva, na mgogoro wa Syria utatuliwe kwa njia ya amani. Pande hizo pia zimekubaliana kuendelea na jitihada za kutimiza lengo la kutokuwa na silaha za nyuklia kwenye Peninsula ya Korea kupitia njia za kidiplomasia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako