• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kuwa Rais mpya wa Liberia

  (GMT+08:00) 2017-12-28 10:03:21

  Baada ya tetesi za muda mrefu hatimaye mshindi pekee wa tuzo ya Ballon D'Or kutoka katika bara la Afrika George Weah amepata kura nyingi zinazomwezesha kunyakua kiti cha uraisi katika uchaguzi uliofanyika nchini Liberia.

  George Weah nyota wa zamani wa Ac Millan ameshinda katika majimbo 12 kati ya majimbo 15 nchini humo akimshinda mpinzani wake wa karibu sana Joseph Boakai.

  Joseph Boakai mwenye umri wa miaka 73 amekuwa makamu wa raisi nchini Liberia kwa muda wa miaka 12 sasa lakini hiyo haikutosha kumpa ushindi kwani aliambulia ushindi majimbo mawili tu.

  Weah amewahi kushinda tuzo ya mchezaji bora Africa mara 3, kombe la Serie A mara 2, Ligue 1 mara 1, FA Cup mara 1 na Ballon D'Or 1 tuzo ambayo hadi sasa hakuna Muafrika mwingine ambaye kaichukua.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako