• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Leila Zerrougui ateuliwa kuwa mjumbe maalumu wa MONUSCO

    (GMT+08:00) 2017-12-28 10:00:01

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres Jumatano amemteua Bibi Leila Zerrougui wa Algeria kuwa mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa Tume ya kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MONUSCO.

    Msemaji wa umoja wa mataifa amesema, Bibi Zerrougui anachukua nafasi ya Bw. Maman Sidikou kutoka Niger, ambaye muda wake utakamilika mwezi Januari mwaka kesho.

    Bibi Zerrougui ana uzoefu wa mambo ya sheria, ulinzi wa raia, usimamizi na uongozi kwa zaidi ya miaka 30. Alikuwa mjumbe maalumu wa katibu mkuu anayeshughulikia mambo ya watoto katika migogoro, kati ya mwaka 2012 na 2016, na naibu mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa kikosi cha MONUSCO kuanzia mwaka 2008 hadi 2012.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako