• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Takriban 20 wauawa katika mapigano ya kikabila Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2017-12-28 10:00:35

    Watu wapatao 20 wameuawa na wengine 18 wamejeruhiwa katika jimbo la Jonglei, kusini mwa Sudan Kusini, baada ya mapigano kuibuka kati ya makundi mawili yanayovutana.

    Waziri wa habari wa Jimbo la Jonglei Bw. Jacob Akech Deng, amesema mapigano yalitokea katika Kaunti ya Bor Kusini mwishoni mwa wiki baada ya makundi mawili kuvutana kutokana na kubadilisha jina la kijiji chao.

    Amesema utulivu umerejea baada ya jeshi na polisi kuunda eneo salama kati ya makundi hayo mawili. Ameongeza kuwa watu saba wanaoshutumiwa kuongoza mapigano hayo wamekamatwa, na watafikishwa mahakamani hivi karibuni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako