• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Thamani ya shilingi ya Kenya dhidi ya dola ya Marekani yashuka

    (GMT+08:00) 2017-12-28 17:53:16

    Shilingi ya Kenya imeendelea kushuka thamani dhidi ya dola ya kimarekani kufuatia mahitaji ya dola ya marekani katika biashara ya mafuta na uagizaji bidhaa kutoka nje huku soko la fedha likiendelea.Wafanya biashara wengi walioongea na Radio China Kimataifa wamesema dola ya Marekani ilinunuliwa kwa shilingi 103 ikilinganishwa na 102 wiki iliyopita.Wakati huo huo serikali ya Kenya imeanza mchakato wa kununua karibu hekari 2000 kutoka kwa wakazi ili kutoa nafasi kwa ujenzi wa awamu ya pili ya mradi wa SGR wa Naivasha. Ardhi hizo zinadaiwa kutafutwa katika kaunti za Kiambu, Kajiado, Nakuru na Narok. katika eneo la Naivasha.Awamu hiyo ya pili inatarajiwa kuchukua muda wa miaka mitatu na utagharimu jumla ya shilingi bilioni 150 ambapo asilimia 90 zitatolewa kama mkopo na benki ya China Exim Bank.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako