• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Cristiano Ronaldo ashinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka katika Tuzo za Dubai Global Soccer 2017

  (GMT+08:00) 2017-12-29 08:42:13

  Tuzo za Dubai Global Soccer 2017 zilifanyika jana usiku huko Dubai na kushuhudia nyota mbalimbali wakiibuka kidedea kwa kutwaa tuzo hizo kwa mwaka 2017, nyota wa soka wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka. Wengine walioshinda tuzo hizo ni kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane ambaye ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwaka 2017 wakati staa wa zamani wa AS Roma Francesco Totti akishinda tuzo ya heshima. Wengine walioshinda tuzo za Dubai Global Soccer Awards 2017 ni pamoja na Jorge Mendes wakala bora 2017, Carlos Puyol tuzo ya heshima 2017, Felix Brych refa bora wa mwaka 2017, Real Madrid wameshinda tuzo ya klabu bora ya mwaka 2017 na tuzo ya kocha bora wa timu ya taifa imeenda kwa kocha wa Misri Hector Cuper.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako