• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wana matarajio mazuri na maendeleo ya Afrika katika mwaka 2018

    (GMT+08:00) 2017-12-29 09:12:27

    Wataalamu wa Rwanda wameonyesha matarajio kuhusu mwelekeo wa Afrika katika mwaka 2018, licha ya bara la Afrika kuendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali.

    Mchambuzi wa mambo ya kisiasa Bw Ladislas Ndengahimana ameliambia shirika la habari la China Xinhua kuwa waafrika sasa wanatambua matatizo yao, hali itakayowasaidia kutafuta ufumbuzi wa ndani.

    Mchambuzi wa mambo ya uchumi Teddy Kaberuka, amesema nchi za Afrika huwa zinaagiza bidhaa nyingi zaidi kuliko zinazouza, hali hii ndio inafanya kuwe na utegemezi wa misaada ya kimataifa kugharamia miradi na bidhaa zinazoagizwa. Amesema Afrika itaendelea kushindwa kuvutia uwekezaji kwenye viwanda kutokana na kutokuwepo kwa utulivu wa kisiasa, usalama na utawala bora.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako