• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia yapata udhibiti wa anga tena baada ya miaka 27

    (GMT+08:00) 2017-12-29 09:44:42

    Serikali ya Somalia imetangaza kuwa imepata udhibiti na usimamizi wa anga, iliyokuwa chini ya udhibiti wa ofisi ya shirika la usafiri wa kiraia la Umoja wa Mataifa (ICAO) iliyoko mjini Nairobi kwa muda wa miaka 27.

    Rais Mohamed Abdulahi Farmajo wa Somalia amezindua ofisi na vifaa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mogadishu na kusema hatua hiyo inawakilisha hatua muhimu kuelekea maendeleo ya nchi hiyo. Ameshukuru juhudi za ICAO, na kusema kurudisha udhibiti wa anga ya Somalia ni sehemu ya ahadi ya serikali ya kurejesha huduma muhimu za umma.

    Waziri wa usafiri wa kiraia wa Somalia Bw. Mohamed Abdulahi Salad, amesema vifaa vyote vya udhibiti wa anga viko tayari na salama, na kwamba serikali imeanzisha tena safari za ndege za moja kwa moja kati ya Mogadishu na Nairobi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako