• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la ndege la Ethiopia lafikiria kuanzisha safari za kwenda Zhengzhou, China

    (GMT+08:00) 2017-12-29 10:08:51

    Shirika la ndege la Ethiopia linafikiria kuanzisha safari za kwenda mji wa Zhengzhou, China.

    Mkurugenzi wa shirika hilo kanda ya China, Mongolia, na Korea ya Kaskazini Bw Yared Berta, amesema mpango wa kuanzisha safari za kwenda mji wa Zhengzhou, Mkoani Henan China, ni sehemu ya jitihada za kuwavutia wateja wapya.

    Bw Berta amesema mji wa Zhengzhou ni moja ya sehemu zinazojulikana nchini China, ambao unavutia uwekezaji mwingi, na kutoa fursa kwa shirika la ndege la Ethiopia haswa kwenye huduma za uchukuzi wa mizigo.

    Hivi sasa Shirika la ndege la Ethiopia linasafirisha abiria 80,000 na tani 60,000 za mizigo kila mwaka kupitia miji tano ya China, ambayo ni Beijing, Hongkong, Shanghai, Chengdu na Guangzhou.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako