• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Libya lakomboa ngome iliyobaki Benghazi

    (GMT+08:00) 2017-12-29 10:09:14

    Jeshi la Libya mashariki mwa nchi Alhamisi lilikomboa eneo la Sidi Ekhrebish, katikati ya mji wa Benghazi, ambayo ni ngome ya mwisho ya magaidi mjini humo, baada ya operesheni iliyodumu kwa zaidi ya miezi mitano.

    kamanda wa vikosi maalumu Jenerali Wanis Boukhamada amethibitisha kuwa Sidi Ekhrebish imekombolewa kabisa na kwamba operesheni za kijeshi zimemalizika. Chanzo cha habari kinasema kikosi kimoja kinaendelea kuwasaka wapiganaji waliokimbia na kuwaua 12 kati yao.

    Chanzo hicho pia kimethibitisha kuwa hakuna askari wa jeshi aliyeuawa, na kusema wapiganaji waliokimbia hawazidi kumi, hakuna uwezekano kwao kufanya mashambulizi dhidi ya jeshi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako