• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yajitahidi kutimiza malengo ya uhifadhi wa mazingira

    (GMT+08:00) 2017-12-29 16:51:09

    Uchafuzi wa mazingira ni moja kati ya matatizo matatu sugu yanayokabili ujenzi wa jamii yenye maisha bora. Mkutano wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC kuhusu kazi za uchumi uliofungwa hivi leo, umeagiza kupunguza utoaji wa uchafuzi kwa kiasi kikubwa, ili kuboresha mazingira, haswa hewa.

    Huu ni mwaka wa mwisho wa utekelezaji wa "mpango wa kukinga na kushughulikia uchafuzi wa hewa". Kutokana na takwimu zilizopatikana hadi sasa, malengo ya mpango huo yatatimizwa kikamilifu. Msemaji wa wizara ya uhifadhi wa mazingira ya China Bw. Liu Youbin anasema,

    "Kuanzia Januari hadi Novemba mwaka huu, kiwango cha uchafuzi wa vumbi aina ya PM10 nchini China kimepungua kwa asilimia 21.5 ikilinganishwa na mwaka 2013 wakati kama huu. Viwango vya uchafuzi wa vumbi aina ya PM2.5 katika sehemu ya Beijing, Tianjin na Hebei, sehemu ya pembetatu ya Mto Yangtze, na sehemu ya pembetatu ya Mto Zhu vimepungua kwa asilimia 38.2, 31.7 na 25.6, huku kiwango hicho cha Beijing pekee kilipungua na kuwa karibu mikrogramu 60 kwa mita moja za ujazo. Wachambuzi wanaona kuwa kutokana na takwimu zilizopatikana na utabiri wa hali ye hewa katika siku tatu zijazo, malengo ya 'mpango wa kukinga na kushughulikia uchafuzi wa hewa' yatatimizwa."

    Mafanikio ya kushughulikia uchafuzi wa hewa yanaonesha kuwa China imepiga hatua kubwa katika juhudi za kuhifadhi mazingira katika miaka kadhaa iliyopita. Licha ya uchafuzi wa hewa, changamoto za uchafuzi wa maji na ardhi pia haziwezi kupuuzwa. Naibu mkurugenzi wa ofisi ya kikundi cha uongozi wa mambo ya uchumi na fedha cha kamati kuu ya CPC Bw. Yang Weimin anasema,

    "Kwa mujibu wa utaratibu wa kushughulikia uchafuzi wa mazingira na utendajikazi katika miaka ya hivi karibuni, tunaweza kupiga hatua dhahiri katika kushughulikia uchafuzi wa hewa kwa haraka, lakini inatuchukua muda mrefu zaidi katika kushughulikia uchafuzi wa maji na ardhi. Kamati kuu ya CPC imeagiza sehemu mbalimbali kutunga mipango inayolingana na hali halisi ya sehemu zao, ili kuboresha mazingira ya jumla hadi kufikia mwaka 2020."

    Mkutano wa kazi za uchumi wa kamati kuu ya CPC umependekeza kurekebisha muundo wa shughuli za uzalishaji, na kuondoa uzalishaji uliopitwa na wakati, na kurekebisha muundo wa matumizi ya nishati na njia za uchukuzi, na kuongeza nguvu ya kubana matumizi ya nishati na ukaguzi kwa juhudi hizi. Naibu mkuu wa taasisi ya utafiti wa sera za maliasili na mazingira ya kituo cha utafiti wa maendeleo ya baraza la serikali ya China Bw. Chang Jiwen anasema,

    "Kutokana na shinikizo la tume ya ukaguzi wa uhifadhi wa mazingira ya kamati kuu ya CPC, baadhi ya sehemu zimefanya kazi nyingi katika kuinua kiwango cha shughuli za uzalishaji, kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa uchafuzi. Katika miaka mitatu ijayo, tunapaswa kuendelea na juhudi za kupunguza uchafuzi kwa mazingira."

    Kutuma tume ya ukaguzi wa uhifadhi wa mazingira ni hatua muhimu ya China katika kuhimiza juhudi za uhifadhi wa mazingira. Tangu mwaka 2015, mikoa 31 ya China yote imefikiwa na kazi za tume hiyo, ambapo matatizo mengi ya uchafuzi wa mazingira yametatuliwa.

    China inajitahidi kupata maendeleo yasiyoleta uchafuzi kwa mazingira. Naibu mkurugenzi wa ofisi ya kikundi cha uongozi wa mambo ya uchumi na fedha cha kamati kuu ya CPC Bw. Yang Weimin anasema,

    "Tunapaswa kutekeleza kwa makini miradi mikubwa ya kufufua mazingira iliyowekwa kwenye mpango wa 13 wa miaka mitano wa maendeleo. Zaidi ya hayo, ni lazima tuanze miradi mipya ya kuboresha mazingira, inayoshirikisha makampuni, mashirikisho na watu binafsi. Tutarekebisha mfumo wa ustaarabu wa uwiano wa viumbe na mazingira, kukamilisha sera ya haki miliki ya maliasili, na kuanzisha utaratibu wa kuhifadhi mazingira wenye mbinu tofauti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako