• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TTCL yatakiwa kuweka utaratibu wa kuepusha vitendo vya uhalifu wa kifedha mitandaoni

    (GMT+08:00) 2017-12-29 18:33:52

    Kampuni ya simu za mkononi Tanzania TTCL imetakiwa kuweka utaratibu thabiti ambao utaepusha vitendo vya uhalifu wa kifedha wa mitandao hasa katika huduma za TTCL Pesa. Akizungumza mjini Dar es Salaam, meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta amesema kampuni hiyo inapaswa kuhakikisha inatoa huduma salama za kifedha ili iweze kuwa mfano wa kuigwa na kampuni nyingine za simu nchini. Alisema TTCL inapaswa kuwa na utaratibu wa kutoa suluhisho kwa wateja wake haraka pindi kunapotokea makosa mbalimbali katika huduma za kifedha. Mbali na hilo, Meya Sitta pia aliitaka kampuni hiyo kumaliza mazungumzo haraka na kampuni nyingine za mawasiliano, ili waweze kusaini makubaliano ambayo yatafanya watumiaji wa TTCL kuweza kupata huduma za kifedha kupitia mitandao mingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako