• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wadau wa sekta ya utalii wataka serikali kudhibiti ujenzi Maasai Mara

    (GMT+08:00) 2017-12-29 18:34:09

    Wadau wa sekta ya utalii nchini Kenya wametaka serikali kudhibiti ujenzi wowote katika kivutio cha utalii duniani Maasai Mara nchini Kenya. Wadau hao wametaja hatua ya serikali ya kaunti ya Narok kusitisha ujenzi wowote katika maeneo hayo haswa sehemu ambazo tayari kuna hoteli za kulala.Afisa mkuu wa sekta hiyo Mohammed Hersi amesema ujenzi kupita kiasi huenda ukaharibu kabisa kivutio hicho cha watalii duniani.Kauli hii inakuja siku chache tu baada ya gavana wa kaunti ya Narok Bw Samuel Tunai kutangaza kuwa serikali yake haitatoa kibali cha ujenzi wowote katika sehemu hiyo.Aliongeza kuwa serikali yake itabomoa baadhi ya mijengo ambayo haijafikia kiwango cha kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako