• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • BOT yaidhinisha bilioni 300 kwa serikali kama mgao wa faida

    (GMT+08:00) 2017-12-29 18:34:26

    Bodi wa wakurugenzi wa benki kuu ya Tanzania BOT imeidhinisha gawio la shilingi bilioni 300 kwa serikali kutokana na faida iliyopatikana kwa mwaka wa fedha 2016/2017.Gavana wa benki kuu ya Tanzania Bwana Benno Ndulu amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kinafanya gawio la BoT katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2014/15 hadi 2016/17 kuwa Sh bilioni 780 ambapo kwa mwaka 2014/15 ilitoa gawio la Sh bilioni 180 na mwaka 2015/16 gawio la Sh bilioni 300. Kifungu cha 18 (5) cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006 kinaipa Benki Kuu mamlaka ya kutoa gawio kwa Serikali pale inapotengeneza faida. Amesisitiza kuwa majukumu ya msingi ya Benki Kuu sio kutengeneza faida, lakini inapotokea kwamba faida imepatikana, sehemu kubwa hutolewa kama gawio kwa Serikali. Majukumu mengine ya BoT ni kuchapisha noti na sarafu za Shilingi ya Tanzania, usimamizi wa mabenki na taasisi za fedha, kusimamia na kudhibiti mifumo ya malipo ya taifa, kuhifadhi akiba ya fedha za kigeni ya taifa, kutoa ushauri wa kiuchumi na fedha kwa Serikali ya Muungano na ya Mapinduzi ya Zanzibar

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako