• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Raia wa DRC wakimbilia Uganda baada ya mashambulizi dhidi ya waasi

    (GMT+08:00) 2017-12-29 18:41:39

    Jeshi la Uganda limesema watu kadhaa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanakimbilia nchini Uganda kwa kuhofia waasi wa ADF kujibu mashambulizi.

    Msemaji wa operesheni ya mashambulizi ya anga na makombora ya masafa marefu iliyopewa jina la "Tuugo", Ronald Kakurungu amesema, wakimbizi hao wanaingia katika wilaya za Bundibugyo, Kasese, na Ntoroko nchini Uganda kutokana na mashambulizi yanayoendelea dhidi ya wapiganaji wa ADF katika mkoa wa Kivu Kaskazini nchini DRC.

    Vyombo vya habari nchini Uganda vimesema, karibu watu 500 wameingia nchini humo kufuatia mashambulizi ya kijeshi katika kambi nane za ADF zilizoko mkoani Kiivu Kaskazini nchini DRC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako