• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yapiga marufuku uuzaji wa Shisha

    (GMT+08:00) 2017-12-29 19:21:25

    Serikali ya Kenya hatimaye imepiga marufuku uuzaji na uvutaji wa Shisha ambayo imethibitishwa kusababisha madhara ya afya.Waziri wa afya wa Kenya Daktari Cleopa Mailu ametangaza kuwa uagizaji wa shisha kutoka nchi za kigeni,utengenezaji wake, uuzaji , usambazaji na utangazaji wake ni marufuku. Hata hivyo hakuna adhabu yeyote iliyotajwa kwa watakaokiuka agizo hilo lakinbi huenda sehemu ya 164 ya sheria za afya itatumiwa kuadhibu wakiukaji. Sehemu hiyo inasema watakaopatikana na hatia watatozwa faini isiyozidi shilingi elfu 50 au kifungo cha miezi sita gerezani au adhabu zote mbili kwa pamoja.Agizo hilo linakuja wiki mbili tu baada ya serikali ya Rwanda kupiga marufuku shisha nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako