• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 10 wauawa katika shambulizi nje ya kanisa nchini Misri

    (GMT+08:00) 2017-12-29 19:40:25

    Watu 10 wameuawa na wengine watano kujeruhiwa katika shambulizi la risasi nje ya kanisa la Mar Mina wilayani Helwan, kusini mwa mji mkuu wa Misri, Cairo.

    Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo imesema, mshambuliaji mmoja aliuawa na mwingine kutoroka kwenye eneo la tukio kwa kutumia pikipiki, na kwamba askari polisi wawili waliuawa katika majibizano ya risasi. Wizara ya afya ya Misri imesema, majeruhi wawili kati ya watano wako kwenye hali mbaya.

    Kikosi cha kutegua mabomu kimetegua mabomu mawili yaliyotegwa karibu na kanisa hilo.

    Hakun kundi lililokiri kuhusika na shambulizi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako