• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pendekezo la China la "Ukanda Mmoja na Njia moja" lasaidia matibabu ya magonjwa ya moyo kwa watoto wa Afghanistan na Mongolia

    (GMT+08:00) 2017-12-30 17:45:15

    Kwa mwaka 2017, China imetoa msaada wa matibabu kwa watoto 74 kutoka nchi za Afghanistan na Mongolia ambao walikuwa wanaugua maradhi ya moyo ya kuzaliwa nayo, taarifa hii ikiwa ni kwa mujibu ripoti ya mwaka ya chama cha msalaba mwekundu cha China.

    Gharama za usafiri pamoja na matibabu ya wagonjwa, wakiwemo 21 kutoka Afghanistan, zilitokana na mfuko maalum wa ushirikiano wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja, zilizotolewa mwezi Februari na mfuko huo mjini Beijing.

    Mfuko huo pia, umesaidia katika shughuli mbalimbali za misaada ya kibinadamu na ndio uliopeleka makundi tisa ya watoa huduma za misaada ya kibinadamu katika nchi za Pakistan, Syria na nyinginezo zilizopo kwenye pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako