• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais mteule wa Liberia aahidi kuboresha maisha ya wananchi

    (GMT+08:00) 2017-12-31 17:26:27

    Rais mteule wa Liberia George Weah, jumamosi hii alisema kuboresha maisha ya watu wa Liberia ndiyo itakuwa kipaumbele chake atakapoingia madarakani mwezi Januari.

    Weah ambaye amezungumza kwa mara ya kwanza tangu atangazwe ijumaa kuwa mshindi wa uchaguzi wa marudio, amesema ataunda serikali ambayo itajikita katika kuboresha maisha ya watu wa Liberia.

    Katika hatua nyingine, mchezaji huyo wa zamani wa mpira wa miguu, amesema wale wote wanaopenda kuwadanganya watu kwa njia za rushwa hawatakuwa na nafasi katika serikali yake.

    Weah amesema utawala wake utajengwa katika misingi ya kitaasisi kama ilivyoanzishwa na Rais Ellen Johnson Sirleaf na amewaita raia wa Liberia walioko nchi za nje warejee kushuhudia maisha mapya na bora.

    Weah atakuwa rais wa 25 wa Liberia pindi atakapoingia madarakani rasmi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako