• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China iko tayari kukuza kuaminiana na kushirikiana na Urusi mwaka 2018

    (GMT+08:00) 2017-12-31 18:28:09

    Rais Xi Jinping wa China amesema yuko tayari kuungana na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, katika kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa na kimkakati na kuendeleza uhusiano wa kivitendo kati ya nchi hizo mbili.

    Rais Xi aliyasema hayo katika ujumbe wa salamu za mwaka mpya aliomtumia Rais Putin.

    Katika ujumbe huo, kwa niaba ya serikali ya China na watu wake, Rais Xi, alituma salamu na kumtakia heri Rais Putin pamoja na raia wa Urusi.

    Amesema China inataka kukuza ushirikiano wa kimakkati wa kimataifa na Urusi kwa ajili ya faida nyingi za kimaendeleo kwa nchi hizo mbili.

    Akijibu ujumbe huo wa salamu, Rais Putin ameahidi kuwa nchi yake itaungana na China katika juhudi za kuimarisha uhusiano wao wa wenzi wa uratibu wa kimkakati wa pande zote na kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako