• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa aitaka dunia mwaka huu iungane kukabiliana na changamoto kuu za dunia

    (GMT+08:00) 2018-01-01 08:50:20

    Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw Antonio Guterres ametoa mwito wa kuwepo kwa umoja katika jumuiya ya kimataifa ili kukabiliana na changamoto kuu na kulinda mambo yanayothaminiwa kwa pamoja.

    Akitoa salamu za kuaga mwaka 2017, Bw Guterres amesema anatoa mwito kuhusu hatari inayoikabili dunia, na kuitaka dunia iungane kutatua migogoro, kuondoa chuki na kulinda mambo yanayothaminiwa kwa pamoja. Amesema kazi hiyo inaweza kufanyika kama nchi mbalimbali zikishirikiana.

    Akizungumzia mwaka uliopita Bw. Guterres pia ametaja changamoto zilizoikabili dunia kama vile wasiwasi kuhusu silaha za nyuklia kuwa mkubwa zaidi tangu ilivyokuwa kama wakati wa vita baridi, madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa yamekuwa ya kutisha zaidi, na kulikuwa na vitendo vya kutisha vya ukiukaji wa haki za binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako