• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Uganda atoa mwito wa juhudi za pamoja kupambana na kundi la ADF

    (GMT+08:00) 2018-01-01 08:56:38

    Rais Yoweri Museveni wa Uganda jana kwenye salamu zake za mwaka mpya, ametoa mwito wa juhudi za pamoja za kikanda kupambana na kundi la ADF lililoko mashariki mwa DRC.

    Rais Museveni amesema nchi za maziwa makuu zinahitaji kutuliza hali ya mashariki ya DRC, ambako kundi la ADF linaendelea kuandikisha na kutoa mafunzo kwa wapiganaji wake.

    Amesema Uganda iko tayari kuingia mkoa wa Kivu Kaskazini wa DRC kusaidia kuondoa waasi hao kama serikali ya DRC itairuhusu kufanya hivyo.

    Tarehe 22 ya mwezi uliopita jeshi la Uganda lilitumia ndege na mizinga kufanya mashambulizi dhidi ya kundi la ADF kwenye misitu ya mkoa wa Kivu Kaskazini, na kuwaua wapiganaji 100 wa kundi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako