• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Rwanda: Mgombea Pekee wa Urais FERWAFA ashindwa

    (GMT+08:00) 2018-01-01 10:09:24

    Katika hali ambayo ni nadra kutokea, Mgombea pekee wa kiti cha Urais katika shirikisho la Mpira wa miguu la Rwanda FERWAFA, Bi. Felicite Rwemalika ameshindwa kupata nusu ya kura zote ili kutangazwa mshindi.

    Mgombea huyo alipata kura 13 kati ya 52, huku kura 39 zikipotea.

    Kutokana na matokeo hayo uchaguzi huo utaitishwa tena katika mkutano mkuu ujao wa FERWAFA na kamati kuu inayomaliza muda wake ikitarajiwa kuendelea na majukumu yake hadi uchaguzi utakapofanyika tena.

    Awali, aliyekuwa Rais wa FERWAFA Vincent Nzamitwa alijitoa dakika ya mwisho katika kinyang'anyiro hicho kwa madai kuwa ni sababu za kifamilia.

    Licha ya kutakiwa kuendelea na majukumu ya Uongozi katika kipindi cha mpito, Nzamitwa hataruhusiwa kugombea tena katika uchaguzi wa marudio.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako