• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Ashley Young wa Manchester United afungiwa kutocheza mechi tatu.

    (GMT+08:00) 2018-01-01 10:11:19

    Mchezaji Manchester United Ashley Young ataalazimika kutocheza mechi tatu mfululizo baada ya kufungiwa na chama cha soka FA.

    FA imemfungia nyota huyo kufuatia kitendo chake cha kumpiga kwa kiwiko cha mkono Dusan Tadic wa Southampton katika mechi baina ya timu hizo mbili iliyoisha kwa sare ya kutofungana jumamosi iliyopita.

    Tukio hilo halikuonwa na moja kwa moja na mwamuzi, lakini kamera za uwanjani hapo zilimnasa na kwa mujibu wa kanuni za FA analazimika kufungiwa.

    Kutokana na adhabu hiyo, Young atakosa mechi ya ligi kuu leo dhidi ya Everton, pia mechi dhidi ya Derby County ya kombe la FA pamoja na mechi nyingine ligi kuu dhidi ya Stoke City.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako