• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Ligi kuu ya Uingereza: Man City yavutwa shati kwa sare ya bila kufungana dhid ya Crystal Palace

    (GMT+08:00) 2018-01-01 10:11:47
    Rekodi ya ushindi katika mechi mfululizo ya Manchester City imehitimishwa jana na Crystal Palace walipolazimisha sare ya bila kufungana kwenye uwanja wa Selhurst Park.

    Licha ya sare hiyo, Man City ambao wameandika rekodi ya kushinda mechi 18 mfululizo ni timu pekee katika ligi hiyo ambayo haijafungwa mpaka sasa na ikiongoza ligi kwa tofauti ya alama 14 dhidi ya Chelsea wanaoshika nafasi ya pili sasa.

    Kutokana na matokeo hayo, kocha wa City Pep Guardiola amesema huenda ikawa vigumu kuifikia rekodi ya kumaliza msimu bila kufungwa hata moja.

    Pia katika mechi hiyo Palace walikosa nafasi adhimu ya ushindi baada ya Luka Milivojevic kukosa penati iliyotokana na rafu ya Raheem Sterling dhidi ya Wilfried Zaha katika dakika za mwisho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako