• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkuu wa CRI atoa salamu za mwaka mpya kwa wasikilizaji duniani

  (GMT+08:00) 2018-01-01 12:57:27

  Wapendwa marafiki,

  Katika wakati huu mzuri wa kuuaga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka 2018, kwa niaba ya Radio China Kimataifa, Shirika la Kimataifa la Radio, Televisheni na Mtandao wa Internet la China, na mimi mwenyewe, nawapa salamu za dhati, na kuwatakia baraka, maisha bora, afya njema na kila la heri katika mwaka mpya.

  Mwaka 2017 ulikuwa ni mwaka wenye maana kubwa kwa China. Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China ulifanyika kwa mafanikio, na kutunga mpango wa maendeleo ya China katika siku zijazo, na pia kuchangia busara na njia za China za utatuzi wa masuala ya kimataifa. Kama rafiki yetu wa mtandao wa Internet Franka Gulin alivyosema, "mkutano huo si kama tu una umuhimu kwa China, bali pia umefuatiliwa sana na dunia nzima. Tukisema China imepata mafanikio makubwa katika miaka mitano iliyopita, basi itapiga hatua kubwa zaidi katika siku za baadaye."

  Katika mwaka uliopita, kutoka kongamano la uchumi wa dunia la Davos, Uswisi, ambalo rais Xi Jinping wa China alitoa kauli ya kujenga "jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya binadamu", hadi mkutano wa kilele kuhusu pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", mkutano wa Xiamen wa nchi za BRICS, na mazungumzo kati ya Chama cha Kikomunisti cha China na vyama vya kisiasa duniani, China imefafanua mapendekezo yake ya kuhimiza amani, maendeleo, kunufaishana na ufungaji mlango, na kuonesha nia ya kujiamini, uvumilivu na kujiwajibika.

  Hivi sasa, hali ya kimataifa na mlingano wa nguvu zinabadilika kwa kina. Utaratibu mpya wa kimataifa katika mambo ya siasa na uchumi unaharakishwa kujengwa, na amani, maendeleo, ushirikiano, mafanikio ya pamoja zimekuwa mkondo usiozuilika wa zama hizi. Tunaamini kuwa mawasiliano ni daraja la kuongeza maelewano na urafiki. Katika mwaka uliopita, CRI ambayo kazi zake kuu ni kurusha matangazo ya lugha za kigeni, matangazo ya ndani, matangazo ya mchanganyiko na matangazo ya ushirikiano, imejitahidi kusonga mbele, na kuelekea kuwa chombo cha habari cha kimataifa cha kisasa na cha aina mpya. Wakati tunapoendeleza shughuli zetu za radio, video, tovuti, gazeti na nyinginezo, pia tunajenga chapa za "China', na kuonesha wasikilizaji wetu hali halisi za China kwa pande zote kupitia APP za simu za mkononi za lugha mbalimbali na software za mawasiliano. Tumetengeneza kwa makini video ndogo, H5, katuni, na maelezo kwa picha kwa wasikilizaji wetu, ili kukidhi mahitaji yao. Tumejitahidi kukamilisha ushirikiano na vyombo vya habari vya nchi za nje, ili CRI iwe chombo cha habari kilichoko karibu na wasikilizaji wetu. Pia tumejaribu njia mpya ya kufanya mawasiliano ya utamaduni na nchi za nje, kwa kuanzisha "maonesho ya tamthilia za China" katika luninga za nchi za nje, ili marafiki zetu wapate njia mpya za kuielewa China.

  Marafiki zetu, mbegu bora haiwezi kuota mzizi na kukua bila ya jua, mvua na rutuba ya ardhi. Hali kadhalika, ikiwa na ufuatiliaji na uungaji mkono wenu, CRI imekuwa na nguvu zaidi ya kusonga mbele. Mwaka jana, idadi ya mawasiliano kati ya wasikilizaji na CRI kwa njia tofauti ilifikia milioni 95, idadi ya mashabiki wa akauti zetu za APP za mawasiliano ilizidi milioni 62, na idadi ya watumiaji wa APP zetu za simu za mkononi ilizidi milioni 26. Idadi hizo zote zimevunja rekodi katika historia. Tunajua kuwa ninyi ni marafiki zetu wapendwa, na barua na maoni kutoka kwenu zinaonesha matumaini na uungaji mkono kwetu. Tafadhali mniruhusu nitoe shukurani kwa marafiki zetu wote kwa niaba ya wafanyakazi wa CRI.

  Kuna msemo wa China unaosema, "mwaka mpya huleta mabadiliko mbalimbali". Mwaka huu, tutatoa huduma bora na kwa wakati za habari, na kuwaletea marafiki zetu majukwaa mengi na mazuri zaidi ya kuielewa China na dunia.

  Nautakia urafiki wetu udumu milele. Nawatekieni kila la heri katika mwaka mpya tena! Asanteni!

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako