• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Afrika Kusini wabadilishana salamu za pongezi za kumbukumbu ya kuanzisha uhusiano kati ya nchi hizo

    (GMT+08:00) 2018-01-01 16:39:13

    Rais Xi Jinping wa China na mwenzake Jacob Zuma wa Afrika Kusini wamebadilishana salamu za pongezi katika kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo.

    Katika ujumbe wake, rais Xi amesema kutokana na juhudi za pamoja katika miaka 20 iliyopita, uhusiano kati ya China na Afrika Kusini umepata maendeleo ya kina na ya pande zote, na umefikia ngazi ya wenzi wa kimkakati wa pande zote.

    Kwa upande wake, rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amesema maadhimisho hayo ni hatua kubwa katika historia ya nchi hizo mbili. Amesema katika miaka 20 iliyopita, China na Afrika Kusini zimepata matokeo makubwa katika ushirikiano kwenye msingi wa urafiki wa jadi na kuaminiana, na kwamba uhusiano wa pande hizo mbili umeimarika na kuwa na umuhimu mkubwa wa kimkakati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako