• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UM ataka dunia iwe na umoja katika mwaka 2018 ili kukabiliana na changamato mbalimbali

    (GMT+08:00) 2018-01-01 16:55:50

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gueterres ametoa mwito kwa jumuiya ya kimataifa kuwa na umoja ili kukabiliana na changamoto.

    Bw. Gueterres ametoa wito huo katika salamu zake za mwaka mpya, ambapo mbali na kuwatakia watu wote duniani heri ya mwaka mpya, amerudia hali ya kukosekana kwa utulivu katika mwaka 2018 na kutaja ongezeko la migogoro, msukosuko wa hali ya hewa na suala la haki za binadamu kama ni vitishio vikubwa vinavyoikabili dunia ya leo. Amesema umoja ni njia pekee ya kutatua changamoto hizo. Anasema,

    "Wakati tunapoingia mwaka wa 2018, natoa mwito wa kuwa na umoja. Naamini tunaweza kuifanya dunia yetu iwe na usalama zaidi, tunaweza kutatua migogoro, kuondoa chuki, kulinda mawazo ya pamoja tuliyo nayo kuhusu thamani, lakini umoja ndio njia yetu pekee. Nawasihi viongozi wa sehemu mbalimbali wafanye nia zao za mwaka mpya kuwa ni kupunguza pengo, kuondoa tofauti, kufikia maoni ya pamoja na kujenga upya hali ya kuaminiana. Umoja ni njia, siku zetu za baadaye zinauhitaji."

    Katika salamu zake, Bw. Guterres pia ametumia lugha za kiingereza, kiarabu, kichina, kifaransa, kirusi, kihispania na kireno kueleza shukrani zake kwa watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako