• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea Kaskazini yataka kupeleka ujumbe kushiriki kwenye michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi

    (GMT+08:00) 2018-01-01 18:16:31

    Kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong Un amesema, nchi hiyo inataka kupeleka ujumbe kushiriki kwenye michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi itakayofanyika nchini Korea Kusini, hivyo kuna uwezekano wa pande mbili za Korea Kaskaizni na Kusini kufanya mazungumzo ya dharura.

    Katika hotuba yake kupitia televisheni, Bw. Kim amesema, mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 70 tangu Korea Kaskazini kuasisiwa, pia Korea Kusini itafanya michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi, hivyo mwaka huu ni muhimu kwa pande zote mbili. Michezo hiyo itakayofanyika nchini Korea Kusini ni fursa nzuri ya kuonesha hadhi ya kikabila.

    Bw. Kim amesema, Korea Kaskazini inapenda kuchukua hatua yoyote ya lazima ikiwemo kupeleka ujumbe, hivyo serikali za pande zote mbili zitaweza kufanya mazungumzo ya dharura. Amesema nchi hizo mbili zina lugha moja na damu moja, hivyo Korea Kaskazini inataka kuiunga mkono na kuisaidia Korea Kusini kufanikisha michezo hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako