• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Serikali yaahidi kukamilisha mradi wa umeme wa REA kwa mda

    (GMT+08:00) 2018-01-01 19:32:15

    NAIBU Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema kuwa wakandarasi walioshindwa kukamilisha miradi ya usambazaji wa umeme vijijini Awamu ya Pili (REA II), watachukuliwa hatua za kisheria na serikali.

    Mgalu alisema hayo jana katika ofi si za wizara hiyo Dar es Salaam katika kikao chake na wakandarasi, wanaotekeleza Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Tanga, inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini.

    Wakandarasi hao ni kampuni ya Derm inayosambaza miundombinu ya umeme katika wilaya za Handeni, Kilindi, Korogwe na Lushoto, Kampuni za Radi, Njarita na Aguila zinazosambaza umeme wilaya za Mkinga, Pangani, Muheza na Bumbuli na kampuni ya Namis Co-operate Ltd inayosambaza miundombinu ya umeme katika wilaya zote za Tanga.

    Kikao hicho pia kilishirikisha watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Naibu Waziri alisema kuwa wakandarasi waliopewa kazi ya kusambaza miundombinu ya kusambaza umeme vijijini kupitia REA Awamu ya Pili, walilipwa malipo yote, hivyo walipaswa kukamilisha miradi yote kwa wakati.

    Aidha, aliwataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA Awamu ya Tatu, kuongeza kasi katika miradi ya usambazaji wa umeme vijijini na kuongeza kuwa kipaumbele kitolewe katika taasisi kama shule, vituo vya afya, zahanati, visima vya maji ili wananchi waanze kufurahia huduma za jamii. Aliwataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA katika mikoa miwili tofauti, kuhakikisha kuwa kasi inakwenda kwa kiwango sawa na kuepuka kuwekeza nguvu kwenye mkoa mmoja tu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako