• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Biashara nzuri msimu wa krismasi kufuatia ongezeko kwa watalii

    (GMT+08:00) 2018-01-01 19:33:14

    Wafanyibiashara nchini Kenya wameandikisha faida kubwa katika msimu wa krismasi na sherehe za mwaka mpya.

    Hoteli za ufuo wa bahari hindi jijini Mombasa na viungani mwake zimeandikisha biashara nzuri msimu huu wa krismasi kufuatia kuongezeka kwa watalii wa kutoka humu nchini ambao wamemiminika jijini humo kusherehekea krismasi .

    Maneja wa mauzo na masoko katika hoteli moja ya Mombasa ,Wafula Waswa amesema biashara imeimarika msimu huu wa krismasi huku mamia ya watalii wakimiminika jijini Mombasa.

    Wafula,alisema hoteli za north coast na south coast zimejaa watalii kufuatia kuzinduliwa kwa huduma za usafiri kwenye reli ya kisasa kati ya Nairobi na Mombasa.

    Terry Gore,mtalii kutoka Denmark alisema ana furahia kusherehekea krismasi ya mwaka wa 30 na mwaka mpya jijini Mombasa kwasababu ya maanthari yake. Gore alitoa wito kwa mataifa ya Ulaya kuwahimiza raia wao kuzuru kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako