• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Treni ya kwanza ya mizigo ya kibiashara yaanza kazi nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2018-01-02 08:31:13

    Treni ya kwanza ya kusafirisha mizigo ya kibiashara iliwasili jana Nairobi ikiwa kwenye ghala la kisasa, ambayo ilizinduliwa na rais Uhuru Kenyatta wiki mbili zilizopita.

    Kwenye taarifa iliyotolewa mjini Nairobi, Mkuu wa Maghala ya makontena ya Bara wa Mamlaka ya bandari ya Kenya Symon Wahome amesema treni mpya ya kusafirisha mizigo italeta mapinduzi kwenye shughuli za usafirishaji mizigo nchini Kenya. Bw. Wahome amesema wakati treni ya mita ilikuwa ikibeba makontena 20 hadi 30, treni ya SGR itakuwa ikibeba makontena 216. Treni ya kusafirisha mizigo inayobeba makontena 104, inakuwa karibu sawa na malori yanayosafiri kila siku kwenye barabara kuu ya Mombasa hadi Nairobi.

    Kuja kwa treni hiyo ya mizigo kunatokana na sera ya serikali ya Kenyatta ya kupunguza gharama za kufanya biashara nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako