• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Libya yaandikisha walinzi wa usalama 500 kwa ajili ya ulinzi na balozi na taasisi za kidiplomasia nchini humo

    (GMT+08:00) 2018-01-02 08:55:13

    Wizara ya mambo ya ndani ya Libya ya serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imeidhinisha kuwaandikisha walinzi wapya 500 wa Idara inayoshughulikia ulinzi wa balozi na taasisi za kidiplomasia nchini Libya.

    Mkuu wa idara hiyo Kanali Wissam Al-Jama amesema walinzi hao watapewa mafunzo mengi kuhusu ujuzi wa mahusiano ya kimataifa.

    Pia alitangaza kuwa balozi kadhaa za nchi za Umoja wa Ulaya zitafunguliwa tena mwanzoni mwa mwaka huu.

    Balozi nyingi za kigeni na tume maalumu ya mashirika ya kimataifa nchini Libya, ikiwa ni pamoja na tume za Umoja wa Mataifa nchini Libya, zilihamia nchi jirani ya Tunisia mwaka 2014 kutokana na vurugu zilizotokea kati ya makundi yenye silaha ya upinzani mjini Tripoli.

    Waziri wa mambo ya nje wa Libya Bw. Mohamed Sayala amesema hadi sasa balozi 30 za kigeni zimefunguliwa tena nchini Libya baada ya kufungwa kwa zaidi ya miaka mitatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako