• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNICEF yataka nchi za Afrika kuhakikisha maisha ya watoto wachanga

    (GMT+08:00) 2018-01-02 09:22:21

    Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF jana lilizitaka nchi za Afrika kuhakikisha watoto wachanga wengi zaidi wanakuwa hai katika siku za mwanzo za maisha yao.

    Taarifa iliyotolewa na UNICEF imekadiria kuwa, karibu watoto elfu 48 watazaliwa katika nchi za Afrika Mashariki na Kusini katika siku ya mwaka mpya.

    Kwa mujibu wa UNICEF karibu asilimia 58 ya watoto wanaozailiwa siku hiyo wako katika nchi tano za kanda hiyo, ambapo watoto 9,023 watazaliwa Ethiopia, 5,995 nchini Tanzania, 4,953 nchini Uganda, 4,237 nchini Kenya na 3,417 nchini Angola.

    Mkurugenzi wa kanda ya Afrika Mashariki na kusini wa UNICEF Leila Pakkala amesema shirika hilo linazitaka serikali na washirika wao kudumisha na kupanua juhudi zao za kuokoa maisha ya watoto kwa kutoa usuluhishi wa uhakika na gharama ya chini.

    Mwaka 2016, takriban watoto 2,600 duniani walikufa ndani ya saa 24 baada ya kuzaliwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako