• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Reli ya kisasa ya Ethiopia hadi Djibouti iliyojengwa na China yaanza huduma za kibiashara

    (GMT+08:00) 2018-01-02 09:23:28

    Reli ya kiilektroniki yenye urefu wa kilomita 756 kutoka Ethiopia hadi Djibouti iliyojengwa na China imeanza rasmi huduma zake za kibiashara baada ya kuzinduliwa mjini Addis Ababa, Ethiopia .

    Akiongea kwenye hafla ya uzinduzi Waziri wa uchukuzi wa Ethiopia Ahmed Shide amesema, mradi huo ni hatua muhimu ya ushirikiano kati ya China na Afrika, ambao si kama tu utaongeza ushirikiano wa kiuchumi na mawasiliano kati ya watu wa Ethiopia na Djibouti, bali pia utachangia sana kwenye juhudi za maendeleo za kuijenga Ethiopia mpya.

    Bw. Shide pia amesifu mchango uliotolewa na China katika kujenga reli hiyo na kuhimiza wakazi wanaoishi karibu na reli kusaidia kudumisha uendeshaji wa reli hiyo.

    Akisisitiza umuhimu wa reli hiyo, balozi wa China nchini Ethiopia Tan Jian, amesema mradi huo utachangia maendeleo ya viwanda na kukuza uchumi wa nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako