• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Salamu za mwaka mpya za rais wa China zapongezwa na wataalamu wa nchi mbalimbali duniani

    (GMT+08:00) 2018-01-02 09:35:20

    Katika mkesha wa mwaka mpya wa 2018, rais Xi Jinping wa China alitoa salamu za mwaka mpya, akikumbusha mafanikio makubwa yaliyopatikana nchini China katika mwaka mmoja uliopita, na kubainisha vipaumbele vya kazi katika mwaka mpya. Salamu hizo zimepongezwa na wataalamu wa nchi mbalimbali duniani.

    Mkuu wa Gazeti la Executive Intelligence Review la Marekani mjini Washington, ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya kimataifa Bw. William Jones amesema, kazi ya kuondoa umaskini, siku zote inachukuliwa kuwa changamoto kubwa zaidi kwa binadamu wote, lakini lengo hili linatimizwa hatua kwa hatua nchini China, hali ambayo imeleta imani kubwa kwa nchi nyingine duniani.

    Mwandishi wa habari wa Gazeti la Pyramid Daily la Misri Bw. Samy Elkamhawy amesema, katika salamu hizo, rais Xi Jinping alisisitiza lengo la kutokomeza umaskini kwa mujibu wa vigezo vya sasa ifikapo mwaka 2020, hali ambayo imeonesha kuwa serikali ya China imefanya utafiti wa kutosha kabla ya kutangaza sera madhubuti. Mwaka huu China imeonesha mwelekeo mzuri wa ukuaji wa uchumi, na kupiga hatua thabiti katika kuangamiza umaskini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako