• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Michezo, Zanzibar: wananchi waishukuru serikali kufautia mafanikio ya kimichezo kwenye mpira wa miguu mwaka 2017

  (GMT+08:00) 2018-01-02 10:32:47

  Wananchi wa Zanzibar wameishukuru serikali kwa kuwa msatri wa mbelee katika kuunga mkono jitihada zinazofanywa na wanamichezo ambapo kipekee wamemwagia sifa RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, na kwamba kwa kuwa ameendelea kuwatia moyo viongozi pamoja na wachezaji.

  Hayo yamesemwa na wananchi wakisifu na kupongeza hotuba ya Rais ya kuukaribisha mwaka 2018 ambayo kwa kiasi kikubwa ilijumuisha mafanikio ya kitaifa yaliyopatikana katika medani za soka kimataifa mwaka 2017 unaagwa huku Zanzibar na kwamba yamerudisha sifa na heshima iliyokuwepo miaka mingi.

  Katika risala yake, Dkt. Sein alizipongeza timu mbili za mpira wa miguu yaani Zanzibar Heroes iliyofanya vyema katika mashindano ya Chalenji nchini Kenya kwa kuwa washindi wa pili na kipekee akiwapongeza Zanzibar Beach Heroes kwa kutwaaa ubingwa wa kimataifa wa soka la ufukweni jijini Dar es Salaam.

  Hivyo, alitoa wito kwa wanamichezo na wananchi wote kushirikiana katika kufufua na kuendeleza michezo nchini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako