• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la anga la Israel lashambulia kituo cha kundi la Hamas kusini mwa Gaza

    (GMT+08:00) 2018-01-02 16:52:20

    Jeshi la anga la Israel mapema leo limeshambulia kituo cha kijeshi cha kundi la Hamas kilicho katika eneo la kusini mwa Ukanda wa Gaza.

    Jeshi la Israel limesema, shambulizi hilo ni kujibu roketi iliyorushwa usiku wa jumatatu na wapiganaji wa Gaza dhidi ya eneo la wazi lililo karibu na Halmashauri ya mkoa wa Eshkol, kusini mwa Israel, lakini hakuna majeraha wala uharibifu ulioripotiwa. Bado hakuna kundi lililotangaza kuwajibika na roketi hiyo, lakini roketi kama hizo hurushwa na makundi ya Kiislamu kutokea Gaza.

    Tangu rais Donald Trump wa Marekani alipotangaza kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel tarehe 6 mwezi Desemba mwaka jana, mapambano kati ya Israel na Gaza yamezidi kuwa makali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako