• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uchumi wa China wakadiriwa kukua kwa asilimia 6.7 mwaka huu

  (GMT+08:00) 2018-01-02 17:24:39

  Ripoti iliyotolewa na idara ya utafiti wa mkakati wa kifedha na kiuchumi iliyo chini ya Taasisi ya Sayansi Jamii ya China imekadiria kuwa mwaka huu, uchumi wa China utaongezeka kwa asilimia 6.7. Pia imependekeza kuendelea kuhimiza mageuzi ya muundo wa utoaji bidhaa kwenye msingi wa kudumisha utulivu wa mahitaji ya ndani ya nchi, na kuimarisha maendeleo endelevu ya uchumi.

  Ripoti inaona kuwa katika robo ya nne ya mwaka 2017, uchumi wa China uliendelea kuongezeka kwa utulivu, uzalishaji wa viwanda ulikuwa tulivu, nguvu mpya za kukuza uchumi ziliendelea kukusanywa. Wakati huohuo, ongezeko la uwekezaji katika mali zisizohamishika, miundombinu, soko la nyumba, na uwekezaji wa raia lilipungua kiasi ikilinganishwa na robo ya tatu ya mwaka jana. Sekta zinazotoa rasilimali na kutengeneza vipuri ziliendelea kupunguza uzalishaji wa kupita kiasi, na baadhi yao zilianza kuongeza uzalishaji wao baada ya kupunguza.

  Mtafiti wa mkakati wa uchumi wa jumla katika idara ya utafiti wa mkakati wa kifedha na kiuchumi iliyoandaa ripoti hiyo Wang Hongju anasema,

  "Tunaona kuwa katika mwaka mzima wa 2017, ongezeko halisi la pato la taifa la China GDP lilikuwa asilimia 6.8 hivi, bei ya manunuzi ya wakazi iliongezeka kwa asilimia 1.6 hivi. Mwaka 2018, tunakadiria kuwa pato la taifa GDP litaongezeka kwa asilimia 6.7, bei ya manunuzi ya wakazi itaongezeka kwa asilimia 2 hivi."

  Bw. Wang pia anaona kuwa katika robo tatu za mwanzo za mwaka jana, uchumi wa dunia ulifufuka kwa kasi zaidi ya ilivyokadiriwa, na uchumi wa Marekani, Ulaya na Japan uliongezeka kwa kasi, soko la ajira liliendelea kuboreka, bei ya bidhaa iliongezeka taratibu. Hata hivyo, Bw. Wang amesema hatari za kisera kutoka nje bado hazipaswi kupuuzwa.

  "Hatari za nje kwa mwaka 2018 zinaweza kutokea baada ya Marekani kupunguza kodi, hatua ambayo kwa muda mfupi itaweza kuongeza kasi ya ongezeko la uchumi wa Marekani, lakini kwa muda mrefu itaweza kutoa athari mbaya kwa pengo la bajeti na madeni yanayoikabili nchi hiyo. Lakini athari ya muda mfupi ni kuwa fedha zitaweza kurudi nchini Marekani."

  Wachambuzi wanaona kuwa katika siku za baadaye China itaendelea kutumia sera zenye ufanisi za mambo ya fedha na sera tulivu za sarafu, kuongeza njia za kudhibiti uchumi wa jumla, kushinda vita katika kuepusha kutokea kwa hatari kubwa, kulenga kwa usahihi sekta zinazosaidia kupunguza umaskini na kutatua suala la uchafuzi wa hewa. Pia itahimiza mageuzi ya ubora, ufanisi na injini. Inatarajiwa kuwa uchumi wa China utaendelea kuongezeka kwa utulivu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako