• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea Kusini yapendekeza mazungumzo ya ngazi ya juu na Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2018-01-02 18:00:04

    Waziri wa masuala ya muungano wa Korea Kusini Cho Myoung-gyon amesema, nchi hiyo imependekeza kufanya mazungumzo ya ngazi ya juu na Korea Kaskazini jumanne wiki ijayo katika kijiji cha Panmunjom.

    Cho amesema anatumaini kuwa nchi hizo zitajadili kwa uwazi masuala yanayofuatiliwa nazo kwa pamoja ili kuboresha uhusiano wao, na pia suala la Korea Kaskazini kushiriki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi itakayofanyika mwezi Februari huko PyeongChang nchini Korea Kusini.

    Wakati huohuo, rais Moon Jae-in wa Korea Kusini amesema nchi yake inakaribisha Korea Kaskazini kutuma ujumbe kushiriki kwenye Michezo hiyo na kufanya mazungumzo kati ya serikali za nchi hizo mbili. Amesema hatua hiyo ni jibu zuri kwa pendekezo la Korea Kusini la kutumia Michezo hiyo kama ni fursa ya kuboresha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Vilevile China imeeleza kupongeza na kuunga mkono juhudi za nchi hizo mbili za kuboresha uhusiano wao, kuhimiza utulivu katika Peninsula ya Korea, na kufanya Peninsula hiyo iwe sehemu isiyo na silaha za nyuklia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako