• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UM aeleza wasiwasi kuhusu vurugu nchini DRC

    (GMT+08:00) 2018-01-02 18:29:22

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ameeleza wasiwasi wake baada ya ripoti kusema vikosi vya usalama vimetumia nguvu kuwatawanya waandamanaji huko Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC na miji mingine, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya watano, wengine kadhaa kujeruhiwa na watu zaidi ya 120 kukamatwa.

    Bw. Guterres ameitaka serikali ya DRC na jeshi lake kujizuia na kuhakikisha uhuru wa kutoa maoni na kufanya maandamano ya amani kwa watu wa nchi hiyo.

    Pia amezitaka pande mbalimbali za kisiasa za nchi hiyo kutimiza kwa pande zote makubaliano ya kisiasa yaliyofikiwa Desemba 31 mwaka 2016, ambayo bado ni njia pekee inayotekelezeka ya kufanya uchaguzi, kukabidhi madaraka kwa amani na kuimarisha utulivu nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako