• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kilele wa FOCAC wa mwaka 2018 kupanga mustakabali wa ushirikiano kati ya China na Afrika katika enzi mpya

    (GMT+08:00) 2018-01-02 18:33:14

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, mkutano wa kilele wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC mwaka huu utafanyika hapa Beijing, China.

    Bw. Geng amesema, katika mkutano huo, viongozi wa China na nchi za Afrika watajadili mpango wa ushirikiano wa kirafiki kati ya pande hizo mbili, na kutunga mustakabali wa ushirikiano kati ya China na Afrika kwenye enzi mpya, ili kutimiza ushirikiano wa kunufaisha pande zote mbili na maendeleo ya pamoja kwenye kiwango cha juu zaidi.

    Ameongeza kuwa mkutano wa kilele utakaofanyika mwaka huu pia utatangaza hatua kubwa zinazolenga kuongoza maendeleo na ushirikiano kati ya China na Afrika na kuhimiza ushirikiano na mawasiliano kati ya pande mbili katika nyanja mbalimbali..

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako