• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Serengeti yaendelea kupata watalii wengi

    (GMT+08:00) 2018-01-02 18:39:52

    Hifadhi kongwe na maarufu ya Serengeti ambayo ni ya pili kwa ukubwa Tanzania, imeendelea kupata watalii wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani, wengi wakiingilia kwenye Uwanja mdogo wa ndege wa Seronera, ndani ya hifadhi hiyo.

    Hayo yamethibitishwa na Ofisa Utalii, Evans Magomba alipokuwa anazungumzia hali ya utalii, huku akisisitiza kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la safari za ndege zinazosafirisha watalii.

    Ongezeko hilo la karibu kila mwaka sasa, linatajwa kusababishwa na mambo mengi, ikiwa ni pamoja na uwepo wa wanyama wa kila aina, lakini pia kuwapo kwa tukio la kipekee duniani na kuhama kwa maelfu ya wanyama aina ya nyumbu kutoka Hifadhi ya Serengeti na kwenda nchi jirani ya Kenya na kisha kurejea nyumbani baada ya mzunguko wa safari ya umbali wa takribani maili 500.

    Katika kuvutia watalii, Hifadhi ya Serengeti ambayo ni moja ya hifadhi maarufu za Tanzania iliyopo chini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), inafuatiwa na Hifadhi ya Ngorongoro na Mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu zaidi barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako