• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Asticom Kenya, yapata ruzuku ya dola milioni 102 kuzalisha kawi safi

    (GMT+08:00) 2018-01-02 18:40:24

    Kampuni ya kuzalisha kawi kutoka kwa takataka ya Asticom Kenya, imepewa ruzuku ya dola milioni 102 kufadhili mradi wa megawati 10 wa kuzalisha kawi katika eneo la Kibera mjini Nairobi.

    Hazina ya Sustainable Energy for Africa inayosimamiswa na benki ya maendeleo ya Afrika AfDB imetoa fedha hizo kugharamia utafiti wa kimazingira na uhadisi wa mradi huo.

    Fedha hizo pia zitatumika kugharamia huduma za ushauri wa kisheria.

    Megawati 10 zitakazozalishwa kutokana na taka zitaungwanishwa kwenye gridi ya taifa.

    Aidha mkuu wa kampuni hiyo ya Asticom Kenya Leah Tsuma amesema bali na kuzalisha kawi watasafisha maji taka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako