• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Wafanyabiashara wafurika Uganda kununua mahindi

    (GMT+08:00) 2018-01-02 18:41:58

    Wafanyabiashara wa nafaka Afrika Mashariki wanafurika nchini Uganda ambako wananunua mahindi kwa nusu bei ya kimataifa huku maeneo mengi kwenye eneo hilo yakikabiliwa na uhaba kutokana na ukame.

    Uganda imeuza karibu tani 38,000 za mahindi za thamani ya dola milioni 15 kwa nchi jirani

    Rwanda kupitia kwa mipaka ya Gatuna na Cyanika imenunua tani 5,405 ikifuatiwa na DRC ambayo imenunua tani 1,105 kupitia mipaka Rusizi, Mpondwe na Rubavu huku mayo Tanzania ikiagiza tani 480.

    Wafanyabiashara wananunua mahindi kutoka maeneo ya Tororo, Gulu, Masindi na Lira kwa bei ya dola 180 kwa tani moja lakini nchini Kenya tani moja imefikia dola 430.

    Hata hivyo uagiziaji huo wa mahindi kwa bei rahisi kutoka Uganda haujapokelewa vyema na wakulima wa Kenya ambao walitarajia watauza bidhaa yao kwa bei zuri.

    Serikali ilikuwa tayari imetenga dola milioni 70 kununua magunia milioni 2.4 ya mahindi kwa ajili ya hifadhi ya kitaifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako