• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Rwanda yaanza kutekeleza sera mpya ya visa

    (GMT+08:00) 2018-01-02 18:42:20

    Rwanda imeanza tarehe 1, 2018 Januari kutekeleza sera yake ya kuwaruhusu wageni wote kupata visa pindi tu wanapoingia nchini humo.

    Kulingana na sera hiyo wageni hawatahitaji kuomba visa kabla ya kusafiri lakini watapewa visa ya siku 30 katika maeneo ya mipakani au kwenye uwanja wa ndege.

    Raia wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki watapewa visa ya miezi sita bila malipo.

    Nchi nyingine ambazo raia wake watapata visa ya siku 90 ni pamoja na Benin, Chad, DRC, Ghana, Guinea, Indonesia, Haiti na Mauritius, .

    Nao raia wa Australia, Ujerumani, Israel, New Zealand, Sweden, Uingereza na Marekani watapewa visa ya siku 30 nakulipa dola 30.

    Hata hivyo idara ya uhamiaji nchini humo imesema visa hiyo sio ya kufanya kazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako