• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yazishutumu nguvu za nje kuchochea maandamano ya kuipinga serikali

    (GMT+08:00) 2018-01-03 09:00:38

    Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei ameonya dhidi ya kile anachokiita "juhudi zote za maadui", ikiwemo kuchochea vurugu na kuiharibu Jamhuri hiyo ya kiislamu. Akizungumzia kwa mara ya kwanza tangu vurugu zitokee Alhamisi wiki iliyopita katika miji mikubwa ya Iran, Ayatollah Khamenei amesema maadui siku zote wanatafuta fursa ya kujipenyeza nchini Iran na kuhujumu nchi hiyo, na amevitaja ushupavu, utiifu na imani ya nchi ya Iran kuwa ni nguvu muhimu za kuzuia hatua hizo za kiadui. Kwa mujibu wa ripoti isiyo kiserikali, mpaka sasa watu 20 wakiwemo raia na maofisa wa usalama, wameuawa kwenye maandamano makubwa yanayoendelea nchini Iran.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako