• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misri kutangaza ratiba ya uchaguzi wa rais utakaofanyika mwaka huu

    (GMT+08:00) 2018-01-03 09:14:41

    Tume ya uchaguzi ya taifa ya Misri (NEA) imesema wiki ijayo itatangaza ratiba ya uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika mwaka huu. Taarifa iliyotolewa na msemaji wa tume hiyo Bw Mahmoud al–Sherif inasema jopo limeundwa kukaribisha maombi kutoka kwa jumuiya zisizo za kiserikali za kitaifa na kimataifa zenye nia ya kufuatilia mchakato wa uchaguzi.

    Amesema hela za kampeni kwa kila mgombea kwenye raundi ya kwanza ya uchaguzi hazitakuwa zaidi ya dola milioni 1.1 za kimarekani.

    Rais wa sasa wa Misri Bw Abdel Fatta al-Sisi, bado haijatangaza kugombea nafasi hiyo, lakini akitangaza anatarajiwa kupata ushindi mkubwa na kuwa hakuna mgombea mwenye nguvu dhidi yake.

    Aliyekuwa waziri mkuu wa Misri Bw Ahmed Shafiq anayeishi uhamishoni nchini Falme za Kiarabu ametangaza nia ya kugombea urais.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako