• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Museveni wa Uganda alionya Shirikisho la Soka la Uganda kutumia vizuri bajeti yake

    (GMT+08:00) 2018-01-03 09:31:35

    Rais Yoweri Museveni wa Uganda amelionya Shirikisho la soka la Uganda kutumia vizuri mapato ya tiketi ya michezo ya soka.

    Rais Museveni amesema shirika hilo lazima liweke mapema mpango mzuri wa bajeti endelevu, na kutumia vizuri mapato hayo. Ameongeza kuwa timu za taifa zinatakiwa kuwa na ustahimilivu na ustadi, na sio kuchoka kwa kukimbia.

    Aidha, rais Museveni ametangaza kwamba timu ya soka ya taifa itapewa basi jipya. Ameahidi kuwa familia za marehemu na majeruhi wa ajali ya basi la timu ya taifa ya Uganda Cranes iliyotokea mwaka 2015, watapewa dola laki 2.9 za kimarekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako