• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mamlaka ya wanyamapori Uganda UWA yakaribisha marufuku ya China dhidi ya biashara ya pembe

    (GMT+08:00) 2018-01-03 09:38:42

    Mamlaka ya wanamapori ya Uganda UMA imepongeza marufuku iliyoanza kutekelezwa na China dhidi ya biashara ya pembe za ndovu na kuitaja kuwa ni hatua muhimu.

    Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka hiyo Bw. Andrew Seguya amesema uamuzi wa China utakwenda mbali zaidi na kusaidia kuwahifadhi tembo wa Afrika.

    Bw. Andrew amesema Uganda inaishukuru serikali ya China kwa kukomesha biashara ya pembe za ndovu, na kusema hatua hiyo imetoa matumaini kwa tembo wa Uganda, tembo wa Afrika na duniani.

    Biashara ya pembe za ndovu nchini China ilikoma rasmi tarehe 31 ya mwezi uliopita, na sasa ni marufuku kuchakata na kuuza pembe za ndovu na bidhaa zake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako